Na Mola wako Mlezi anawajua vilivyo waliomo mbinguni na katika ardhi. Na hakika tumewafadhilisha baadhi ya Manabii kuliko wengine; na Daudi tulimpa Zaburi. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na Mola wako, ewe Mtume, Anawajua zaidi walioko mbinguni na ardhini, na tumewafadhilisha baadhi ya Mitume juu ya wengine kwa matukufu, wingi wa wafuasi na kuwateremshia Vitabu, na Dawud, amani imshukiye, tumempa Zaburi.